Serikali
imeamua kutoa elimu pasipo malipo kwa elimu msingi kuanzia elimu ya
awali hadi kidato cha nne,kuanzia mwaka wa masomo wa 2016.
Azima hii ya serikali ni katika kutekeleza sera ya Elimu na Mafunzo ya
mwaka 2014 ambayo ina lengo la kuhakikisha kwamba watoto wote wa
Tanzania wanapata Elimu bila kikwazo ikiwemo ada au malipo.
Katika kutekeleza maamuzi hayo,ada zote zilizokuwa zikilipwa kwa ajili
ya elimu ya kidato cha kwanza hadi cha nne zimefutwa.Pia, waraka wa
Elimu namba 8 wa mwaka 2011 kuhusu michango shuleni nao pia umefutwa.
Aidha, mwongozo wa elimumsingi bila malipo unaandaliwa na utatumwa kwa
wamiliki wa shule ifikapo au kabla ya tarehe 15 Disemba 2015.
Waraka huu umeanza kutumika tarehe 21 Novemba 2015
Saturday, November 28, 2015
HUU NDIO WARAKA KUHUSU UTOLEWAJI WA ELIMU BURE KUANZIA FORM 1-4 JANURAY 2016
MASWAYETU EXCLUSIVE BLOG
Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0768 260834. Soma Zaidi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
POST A COMMENT