TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA IKULU | BULOMBORA YETU BLOG
Breaking News
Loading...

Saturday, November 28, 2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA IKULU

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telegrams : "CABINET"
DAR ES SALAAM
Telephone : 2116898, 2116900/6
E-mail : chief@ikulu.go.tz
E-mail : ikulu@ikulu.go.tz
Fax : 2113425/2116914/2117272
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD
11400 DAR ES SALAAM.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ametoa ufafanuzi wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu kupunguza matumizi yasiyo yalazima katika Wizara, idara na taasisi za serikali.
Katika ufafanuzi huo Balozi Sefue amemtaka kila Mtendaji Mkuu ama Afisa Masuhuli wa serikali kujiuliza mwenyewe ni kwa kiasi gani anatekeleza kwa vitendo nia ya Rais ya kuepuka matumizi yasiyo ya lazima.
"Rais ameonesha njia ya kubana matumizi yasio ya lazima, sasa kwa wakati huu ni vema kila Mtendaji Mkuu wa Serikali, ajiulize endapo Rais Magufuli atafika katika eneo langu la kazi, ni kwa kiasi gani atakuta nimetekeleza maagizo yake?" amesisitiza Balozi Sefue.
Kutokana na ufafanuzi huo Balozi Sefue pia amezungumzia Uchapishaji wa Kalenda na vitabu vya kumbukumbu yaani "Diaries" akisema Kila Mtendaji Mkuu wa serikali ama Afisa Masuhuli apime mwenyewe kama ni lazima kutengeneza na kuchapisha Kalenda na Diary? na kama ni lazima achapishe kwa kiasi gani?
"Ni matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kila Wizara, Idara na Taasisi za serikali kuchapisha idadi kubwa ya Kalenda na Diaries ambazo wakati mwingine hata hazitumiki mpaka mwaka unakwisha" ameongeza Balozi Sefue.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam, Novemba 28, 2015

google+

linkedin

MASWAYETU EXCLUSIVE BLOG
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0768 260834. Soma Zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    IDADI YA WASOMAJI