Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu amefanya Mabadiliko kwa
baadhi ya Makamanda wa Polisi wa mikoa na vikosi hapa nchini.
Mabadiliko
hayo ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Kamishna
Msaidizi Mwandamizi SACP Leonard Paul amehamishwa kwenda kuwa Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tanga na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna Msaidizi
Mwandamizi SACP Ulrich Matei aliyekuwa Mkuu wa Utawala Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam.
Kamishna
Msaidizi wa Polisi ACP Mihayo Msikhela aliyekuwa kamanda wa Polisi
mkoa wa Tanga amehamishwa kwenda kuwa Mkuu wa Kikosi cha Kuzuia dawa za
kulevya.
Aliyekuwa
Kamanda wa Polisi mkoa wa kilimanjaro Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP
Ramadhani Mungi anaenda kuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Bandari na
nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Wilbrod
Mtafungwa ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe.
Aliyekuwa
Afisa mnadhimu Mkoa wa Iringa Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP
Prudenciana Protas anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe.
Aliyekuwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Philipo
Kalangi amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi na nafasi inachukuliwa na
aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Shinyanga ACP Ramadhan Ng’azi.
Aidha,
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP
Camilius Wambura anakwenda kuwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar
es Salaam na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP
Francis Massawe kutoka Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam.
Aliyekuwa
Afisa Mnadhimu Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Gilles
Mroto anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya
kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Gemini Mushi
aliyehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam.
Wengine
ni pamoja na Naibu Kamishna wa Polisi DCP Hezron Gimbi anayetoka
Upelelezi Makao Makuu Dar es Salaam kwenda kuwa Mkuu wa Utawala Kanda
Maalumu Dar es Salaam pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP
Costantine Massawe anakwenda kuwa Mkuu wa Oparesheni wa Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam.
Mabadiliko hayo ni ya kawaida kwa mujibu wa Sheria, kanuni na taratibu za Jeshi la Polisi.
Imetolewa na:
Advera Bulimba-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi (T)
Makao Makuu ya Polisi.
0 comments:
POST A COMMENT