
RAIS John Magufuli amesema nchi bado inakabiliwa na tatizo la imani za
kishirikina dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi kufanyiwa vitendo
kinyume na haki za binadamu, ikiwemo kuuawa na kueleza kuwa
kinachotakiwa ni kubadilisha mitazamo ya watanzania kuhusu albino. Aidha,
kukosekana kwa taarifa, ushahidi pamoja na ushahidi wa kimahakama wa
matukio wanaofanyiwa albino ni changamoto nyingine...