KIDOA KUWINDWA NA KIGOGO KWA MIL 10 | BULOMBORA YETU BLOG
Breaking News
Loading...

Saturday, November 28, 2015

KIDOA KUWINDWA NA KIGOGO KWA MIL 10



89Video Queen mwenye mvuto wa aina yake, Asha Salumu ‘Kidoa’.
Mwandishi wetu
FEDHA inaongea! Kigogo mmoja aliyeomba jina lake lihifadhiwe, amedaiwa ‘kukolea’ kimahaba kwa Video Queen mwenye mvuto wa aina yake, Asha Salumu ‘Kidoa’ kiasi cha kutangaza dau la shilingi milioni kumi.
63Chanzo chetu makini kilicho beneti na kigogo huyo anayemiliki yadi kadhaa za magari hapa Bongo, kimesema bosi huyo kila wakati amekuwa akimzungumzia Kidoa na kuahidi kumpa shilingi milioni kumi endapo tu atafanikiwa kulipata penzi lake.
Chanzo hicho kilikwenda mbali zaidi na kusema kwamba kigogo huyo amekuwa akihaha kila kona kutafuta namba za simu za Kidoa ili aweze kuzungumza naye na kuelewana na hatimaye kumpa malavidavi.
81
“Jamaa yangu amechanganyikiwa mno, hatulii, kila wakati anamuulizia Kidoa huku akiahidi kumpatia milioni kumi kama tu atafanikiwa japo kuwa naye usiku kucha kwani kama mademu kaona wengi, ila kwa Kidoa, moyo wake umegota kabisa. Kila siku anahaha kutafuta namba yake, hajaipata ila yupo radhi kuinunua kwa gharama yoyote ile,” kilisema chanzo hicho.
Mara baada ya kunyetishiwa ubuyu huo, mwanahabari wetu alimvutia waya kigogo huyo ambapo alikiri kumsaka mrembo huyo kwa hali na mali lakini akaomba asiandikwe gazetini.
“Jamani kama mnaweza mnisaidie. Mtoto kaumbika, nilianza kumuona kwenye ile video ya Akadumba ya Nay wa Mitego sasa picha zake zinazotoka katika magazeti zinanidatisha kweli nisaidieni ila ‘please’ msiniandike gazetini,” alisema kigogo huyo.

google+

linkedin

MASWAYETU EXCLUSIVE BLOG
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0768 260834. Soma Zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    IDADI YA WASOMAJI