Naibu
Katibu Mkuu Chadema, Salum Mwalimu akionyesha kibali kilichotolewa na
Manispaa ya Ilemela ili kuruhusu ibada ya kumuaga Marehemu Mawazo
Kufanyika kesho katika Uwanja wa Furahisha
Mkutano wa Naibu Katibu Mkuu Chadema Salum Mwalimu na Wanahabari Jijini Mwanza.
Kushoto ni Ezekiel Wenje na Kulia ni Grace Kihwelu ambae ni Mbunge Viti Maalumu Chadema Mkoani Kilimanjaro
Singo
Kigaila Benson ambae ni Mkurugenzi wa Mafunzo Chadema (Kushoto) akiwa
na Peter Mekele ambae ni Mwenyekiti Chadema Kanda ya Ziwa Victoria
(Kulia)
Husna Amri Said ambae ni Mwenyekiti BAWACHA Wilayani Geita
Viongozi na Makada wa Chadema
Mkutano wa kutoa ratiba za kuuaga mwili wa Marehemu Mawazo kwa wanahabari Jijini Mwanza jana.
Mkutano wa Naibu Katibu Mkuu Chadema Salum Mwalimu na Wanahabari Jijini Mwanza jana.
Wanahabari
Na:Binagi Media Group
Mwili wa aliekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mkoa wa Geita Marehemu Alphonce Mawazo, leo unatarajiwa kuagwa katika Viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza kabla ya kusafirisha kwenda Mkoani Geita humo kwa ajili ya Mazishi.
Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema Salum Mwalimu, alisema Marehemu Mawazo ataagwa Kitaifa kwa taratibu za chama hicho, katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.

Alisema ratiba hiyo itatanguliwa na ratiba ya kifamilia ya
kuuaga mwili huo, ambayo itafanyika asubuhi Nyegezi Jijini Mwanza ambako
ni nyumbani kwa Mchungaji Charles Lugiko ambae ni baba mdogo wa
Marehemu Mawazo hiyo ikiwa ni baada ya mwili wake kutolewa katika
Hospitali ya Rufaa Bugando ulikohifadhiwa.
Mwalimu amebainisha kwamba mwili huo utasafirishwa kwenda Mkoani Geita kuanzia majira ya saa nane mchana ambapo wakazi wa Mkoa huo pia watapata fursa ya kuuaga kesho kutwa jumapili.
Allieleza kwamba kuanzia majira ya saa mbili asubuhi, shughuli za kuuaga mwili huo zitafanyika Kimkoa katika Uwanja wa Magereza Mjini Geita na baadae kusafirisha kwenda Katoro ambapo wakazi wa Jimbo lake la Busanda watapata fursa ya kuuaga mwili huo.

Mwalimu aliongeza kuwa, baada ya shughuli zote hizo kukamilika,
mazishi ya Marehemu Mawazo yanatarajiwa kufanyika siku ya
Jumatatu katika Kijiji cha Chikobe Jimbo la Busanda Mkoani Geita.
Shughuli zote hizo zinatarajiwa kuongozwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe, Viongozi waandamizi wa Chama hicho akiwemo Frederick Sumaye, aliekuwa mgombea urais wa Ukawa Edward Lowasa, wabunge pamoja na makada wa Chadema.
Ratiba za Mazishi ya Marehemu Mawazo ambae aliuawa Novemba 14 mwaka huu na watu wasiojulikana, zimejiri baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza jana kuondoa zuio la Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza, lililokuwa zinazuia mwili huo kuagwa Jijini Mwanza kutokana na hofu ya kiusalama pamoja na uwepo wa mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambapo zuio hilo liliondolewa katika kesi
iliyofunguliwa na baba mlezi wa Mawazo, Mchungaji Charles Lugiko baada mvutano mkali wa siku nne mahakamani hapo.

0 comments:
POST A COMMENT