WAKAZI wa Jiji la Mwanza na vitongoji vyake wametakiwa kujitokeza kwa
wingi keshokutwa ili kumpokea Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye
anatarajiwa kuwasili jijini hapa akitokea jijini Dar es Salaam akielekea
mkoani Simiyu.
Hayo yameelezwa jana jijini hapa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,
Baraka Konisaga ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, wakati
alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara wa Kamanga Feri wakati
alipowaongoza kwenye shughuli ya kufanya usafi.
“Niwataarifu kuwa Waziri Mkuu atawasili jijini Mwanza kwa mara ya
kwanza siku ya Jumanne majira ya saa 7:00 mchana akitokea jijini Dar es
Salaam… akishawasili hapa ataelekea mkoani Simiyu kikazi, nawaomba
muiweke moyoni siku hiyo ya Jumanne na mjitokeze kwa wingi kumlaki
kiongozi wetu mpendwa, ” alisema.
0 comments:
POST A COMMENT