JOYCE
Ndalichako, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi,
amewasimamisha kazi watumishi watatu wa Bodi ya Taasisi ya Elimu nchini
(TET) kwa kushindwa kusimamia sheria ya manunuzi na kazi ya uchapaji
wa vitabu ili kupisha uchunguzi
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kwa niaba ya Waziri wa
Elimu, Maimuna Tarishi ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, amesema
watumishi hao hawakutekeleza majukumu yao ipasavyo na kuruhusu vitabu
hivyo kuchapishwa vikiwa na mapungufu.
“Mnamo
tarehe 22 Januari mwaka 2016 bodi hiyo ilishauriwa kusitisha uchapaji
wa vitabu uliokuwa ukifanywa na kampuni ya Yukos Enterprises Ltd baada
ya kubainika kuwa na mapungufu, lakini haikusitisha,” amesema Tarishi na kuongeza.
“Serikali
iliamua kusitisha uchapishaji wa vitabu hivyo ili isiendelee kupokea
vitabu vyenye mapungufu, hata hivyo taasisi ya elimu haikusitisha
uchapishaji wa vitabu hivyo, badala yake kampuni hiyo ilichapisha vitabu
vyote ilivyopangiwa,” amesema Tarishi.
Tarishi
amesema ufuatiliaji uliofanywa na wizara katika bohari ambayo ilikuwa
inapokea vitabu hivyo, ulibaini kuwa vitabu vilivyowasilishwa na kampuni
ya Yukos vilikuwa na kasoro.
“Kutokana
na kasoro hizo, Taasisi haikutekeleza wajibu wake wa kusimamia uchapaji
wa vitabu na uzingatiaji wa sheria ya manunuzi kikamilifu,” amesema.
Kutokana
na mapungufu hayo, Wizara imetoa maagizo ya kuondolewa kwa baadhi ya
vitabu vilivyowasilishwa kwenye bohari ya serikali ifikapo tarehe 29
Februari mwaka huu.
“
Taasisi ya Elimu iwasimamishe kazi mara moja watumishi wafuatao ambao
walikuwa na jukumu la kusimamia sheria ya manunuzi na kazi ya uchapaji
wa vitabu ili kupisha uchunguzi,” amesema.
Amewataja
watumishi hao kuwa ni Peter Bandio, aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa
Idara ya Vifaa vya Kielimu, Pili Magongo Mwanasheria wa TET na Jackson
Mwaigonela Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi na Ugavi.
Mapungufu
yaliyoonekana kwenye vitabu hivyo ni upungu wa mwingiliano wa rangi,
upungufu wa kurasa katika vitabu, ukataji usiozingatia vipimo,vitabu
kuchakaa kabla ya matumizi na mpangilo mbaya wa kurasa.
0 comments:
POST A COMMENT