BULOMBORA YETU BLOG

BULOMBORA YETU BLOG

Breaking News
Loading...

Latest Post

Saturday, February 27, 2016

Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako Awasimamisha Kazi vigogo watatu taasisi ya elimu


JOYCE Ndalichako, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, amewasimamisha kazi watumishi watatu wa Bodi ya Taasisi ya Elimu nchini (TET) kwa kushindwa kusimamia   sheria ya manunuzi na kazi ya uchapaji wa vitabu ili kupisha uchunguzi

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Maimuna Tarishi ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, amesema watumishi hao hawakutekeleza majukumu yao ipasavyo na kuruhusu vitabu hivyo kuchapishwa vikiwa na mapungufu.

“Mnamo tarehe 22 Januari mwaka 2016 bodi hiyo ilishauriwa kusitisha uchapaji wa vitabu uliokuwa ukifanywa na kampuni ya Yukos Enterprises Ltd baada ya kubainika kuwa na mapungufu, lakini haikusitisha,” amesema Tarishi na kuongeza.

“Serikali iliamua kusitisha uchapishaji wa vitabu hivyo ili isiendelee kupokea vitabu vyenye mapungufu, hata hivyo taasisi ya elimu haikusitisha uchapishaji wa vitabu hivyo, badala yake kampuni hiyo ilichapisha vitabu vyote ilivyopangiwa,” amesema Tarishi.

Tarishi amesema ufuatiliaji uliofanywa na wizara katika bohari ambayo ilikuwa inapokea vitabu hivyo, ulibaini kuwa vitabu vilivyowasilishwa na kampuni ya Yukos vilikuwa na kasoro.

“Kutokana na kasoro hizo, Taasisi haikutekeleza wajibu wake wa kusimamia uchapaji wa vitabu na uzingatiaji wa sheria ya manunuzi kikamilifu,” amesema.

Kutokana na mapungufu hayo, Wizara imetoa maagizo ya kuondolewa kwa baadhi ya vitabu vilivyowasilishwa kwenye bohari ya serikali ifikapo tarehe 29 Februari mwaka huu.

“ Taasisi ya Elimu iwasimamishe kazi mara moja watumishi wafuatao ambao walikuwa na jukumu la kusimamia sheria ya manunuzi na kazi ya uchapaji wa vitabu ili kupisha uchunguzi,” amesema.

Amewataja watumishi hao kuwa ni  Peter Bandio, aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Vifaa vya Kielimu, Pili Magongo Mwanasheria wa TET na Jackson Mwaigonela Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi na Ugavi.

Mapungufu yaliyoonekana kwenye vitabu hivyo ni  upungu wa mwingiliano wa rangi, upungufu wa kurasa katika vitabu, ukataji usiozingatia vipimo,vitabu kuchakaa kabla ya matumizi na mpangilo mbaya wa kurasa.

Waziri Mkuu Kutua Jijini Mwanza Kesho Kutwa


WAKAZI wa Jiji la Mwanza na vitongoji vyake wametakiwa kujitokeza kwa wingi keshokutwa ili kumpokea Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye anatarajiwa kuwasili jijini hapa akitokea jijini Dar es Salaam akielekea mkoani Simiyu.
 
Hayo yameelezwa jana jijini hapa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Baraka Konisaga ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, wakati alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara wa Kamanga Feri wakati alipowaongoza kwenye shughuli ya kufanya usafi.
 
“Niwataarifu kuwa Waziri Mkuu atawasili jijini Mwanza kwa mara ya kwanza siku ya Jumanne majira ya saa 7:00 mchana akitokea jijini Dar es Salaam… akishawasili hapa ataelekea mkoani Simiyu kikazi, nawaomba muiweke moyoni siku hiyo ya Jumanne na mjitokeze kwa wingi kumlaki kiongozi wetu mpendwa, ” alisema.

Ripoti Ya Polisi Kuhusu Tukio la Ujambazi Mbagala: Waliofariki Dunia ni Watu 7........Kati Yao Majambazi ni 3, Askari 2 na Raia 2



Ujambazi wa kutumia vifaa vya kivita umeibuka jijini Dar es Salaam, ukiwemo uliofanyika katika uporaji wa Benki ya Access juzi, ambako majambazi walitumia bunduki za kivita aina ya SMG na mabomu ya kurusha kwa mkono.

Akizungumza jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro, alisema mbali na uvamizi huo, pia Polisi imebaini na kukamata askari bandia, waliokuwa na sare rasmi za Jeshi la Polisi zenye vyeo na redio call, zenye uwezo wa kuingilia mawasiliano ya askari Polisi.

Akizungumzia matukio hayo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga alisema atakutana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi, ili Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Polisi, waanzishe msako wa pamoja dhidi ya wahalifu hao.

Uvamizi, mauaji Mbagala
Akisimulia ujambazi uliofanyika katika Benki ya Access Tawi la Mbagala, Kamanda Sirro alisema majambazi hao walikuwa 12, wakiwa wamepakizana kwenye pikipiki sita na walifika kwenye benki hiyo saa 8:30 mchana.

Baada ya kufika, moja kwa moja waliingia kwenye chumba cha askari wanaolinda benki na kumpiga risasi kichwani askari mwenye namba H7739 Konstebo Harid na kufa papo hapo.

Mbali na mauaji hayo, Kamanda Sirro alisema walimshambulia askari mwingine, Konstebo Shaban miguuni na kupora silaha zao na kuingia nazo ndani ya benki, ambako walimshambulia mlinzi wa kampuni binafsi ya ulinzi na raia wengine wawili na kufa papo hapo, huku wengine watano wakijeruhiwa.

Baada ya hapo kwa mujibu wa Kamanda Sirro, majambazi hao walikimbilia chumba kinachohifadhi fedha nyingi (strong room) na kukipiga risasi katika jitihada ya kutaka kuingia ndani, lakini hawakuweza kuvunja.

Kutokana na ugumu wa kuvunja chumba hicho, Kamanda Sirro alisema haraka haraka wakahamia katika kaunta za watoa fedha na kupora fedha zilizokuwepo kati ya Sh milioni 20 mpaka Sh milioni 30 na kuondoka na silaha za polisi aina ya SMG mbili na ile yao moja pamoja na pikipiki zao.

Polisi waua watatu
Kamanda Sirro alisema taarifa zilisambazwa katika vikosi vya ulinzi, ambavyo vilijiimarisha.

Alitaja Kikosi cha Mbwa na Farasi eneo la Mkuranga, ambao walijiandaa na majambazi hao walipofika kijiji cha Chui wilayani Mkuranga mkoani Pwani, walipambana na polisi na askari wakafanikiwa kuua majambazi watatu.

Mbali na kuua watatu, silaha tatu zilikamatwa ambazo ndio zile SMG mbili za Polisi, walizochukua pamoja na ile yao moja, lakini wakakutwa pia na mabomu matatu ya kutupa kwa mkono yaliyotengenezwa Urusi.

“Hawa majambazi walikuwa wamejiandaa, kwa maana walikuwa na mabomu ya kutupwa kwa mkono matatu aina ya RGD 01 ambayo ni mbinu ya kujilinda wanaposhambulia,” alisema Kamanda Sirro.

Tisa watoroka
Pamoja na kujiimarisha kwa polisi, majambazi tisa walikimbia wakaacha pikipiki zote sita za aina tofauti, ambazo ni Haojue mbili zenye namba MC 560 AED na MC 207 BAN, San LG yenye namba MC 784 BDJ, Boxer yenye namba MC 248 AXE na King Lion mbili zenye namba MC 653 BDQ na MC 853 BDR.

Kamanda Siro alisema baada ya hapo, waliendelea kuwakimbiza majambazi hao hadi wakatokomea katika Msitu wa Kongowe, ambako juhudi za kuwatafuta zilianza mara moja.

“Nawahakikishia wananchi mtandao wote wa ujambazi kwenye mabenki na maeneo mengine, tutausafisha wote kwa maana hawa wanafanya uhalifu maeneo ya Dar es Salaam na Pwani na wana ndugu zao, tutawakamata wote,” alisisitiza Kamanda Sirro.

Alisema hawawezi kuona Watanzania wakiumia na kufa kwa tamaa za wachache, wenye kupenda utajiri wa haraka.

JWTZ kazini
Akizungumza kuhusu ujambazi huo, Waziri Kitwanga alisema Polisi inajipanga upya na atazungumza na Waziri mwenzake, Dk Mwinyi kuangalia jinsi ya majeshi hayo mawili, Jeshi la Polisi na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), watakavyofanya kazi pamoja ya msako katika misitu yote inayozunguka mikoa ya Pwani, kuanzia Bagamoyo hadi Kisarawe.

Alionya kama kuna kambi za uhalifu ndani ya misitu hiyo, zitasambaratishwa na kuomba raia wema watoe taarifa za uhalifu.

“Tutafanya operesheni kubwa na tutaifanya haraka, tunaomba wananchi watoe ushirikiano hasa waendesha bodaboda kwa maana zinatumika sana kwenye matukio haya. Mtandao wa majambazi ufahamu kwamba vyombo vya usalama havijalala, tutawamaliza wote, tutatumia nguvu zetu zote kuwamaliza na tutafanikiwa,” alisisitiza Kitwanga.

Kuhusu waendesha bodaboda, Kitwanga alisema ukaguzi wa kina unafanywa na kuwataka waendesha bodaboda hao wanaposimamishwa, wakubali na kutoa ushirikiano na wasione kama wanabughudhiwa, bali ni kuwakagua kwa sababu wahalifu hutumia vyombo hivyo zaidi kufanya matukio mabaya.

Polisi feki
Katika tukio jingine, Kamanda Sirro alisema polisi feki wanne wamekamatwa na wanashikilia kwa mahojiano, ili kubaini mtandao huo ambao unatumia sare za Polisi, redio za upepo na pingu kufanya matukio ya uhalifu.

Alisema walipata taarifa kutoka kwa raia wema ya kuwepo kwa mtandao wa askari bandia, ambao hutumia sare za jeshi hilo kufanya matukio ya uhalifu, ndipo walipowakamata hao wanne.
Kwa mujibu wa Kamanda Sirro, polisi feki watatu walikamatwa Februari 24, asubuhi saa mbili eneo la Upanga karibu na Daraja la Selander.

Alisema watuhumiwa hao baada ya kuhojiwa, walikiri kufanya matukio ya ujambazi kwa kutumia silaha na kumtaja mtuhumiwa mwenzao mmoja anayeishi Kinyerezi.
Kamanda Siro alisema Polisi walimfuata mtuhumiwa huyo nyumbani kwake Kinyerezi na walipofanya upekuzi, walimkuta na sare halisi ya Polisi, redio ya upepo na pingu.

Kamanda Sirro alisema baada ya uchunguzi, imebainika kwamba watuhumiwa hao wamekuwa wakitumia sare na vifaa hivyo vya Polisi, kufanya matukio mbalimbali ya ujambazi kwa kujiaminisha kuwa wao ni askari Polisi.

Alisema watuhumiwa hao wamekiri kufanya matukio mbalimbali, ikiwemo kuweka vizuizi katika barabara za mikoani na kufanya uporaji.

“Watuhumiwa hao wote wanahojiwa ili waeleze jinsi walivyopata sare na vifaa hivyo ya Polisi, wamekiri kufanya uhalifu maeneo mbalimbali, lakini wakati mwingine tunashindwa kukamata wahalifu kwa sababu redio call wanayotumia zinaingiliana na zetu, hivyo wanakuwa wamepata taarifa,” alisema Kamanda Sirro.

Katika tukio lingine, Februari 18 mwaka huu, watuhumiwa watatu wa ujambazi, walikamatwa eneo la Kiwalani Kwa Mkude jijini Dar es Salaam wakiwa na bastola moja.

IGP Afanya Mabadiliko Ya Makamanda Wa Polisi Kwa Baadhi Ya Mikoa



Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu amefanya Mabadiliko kwa baadhi ya Makamanda wa Polisi wa mikoa na vikosi hapa nchini.

Mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Leonard Paul amehamishwa  kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Ulrich Matei aliyekuwa Mkuu wa Utawala Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.  
Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Mihayo Msikhela  aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga amehamishwa kwenda kuwa Mkuu wa Kikosi cha Kuzuia dawa za kulevya. 
 
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa kilimanjaro Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Ramadhani Mungi anaenda kuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Bandari na nafasi yake inachukuliwa na   Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Wilbrod Mtafungwa ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe. 
 
Aliyekuwa Afisa mnadhimu Mkoa wa Iringa Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Prudenciana Protas anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe. 
 
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Philipo Kalangi amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi na nafasi inachukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Shinyanga ACP Ramadhan Ng’azi.   
 
Aidha,  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Camilius Wambura anakwenda kuwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam  na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Francis Massawe kutoka Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam. 
Aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Gilles Mroto anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Gemini Mushi aliyehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam. 
 
Wengine ni pamoja na Naibu Kamishna wa Polisi DCP Hezron Gimbi anayetoka Upelelezi Makao Makuu Dar es  Salaam kwenda kuwa Mkuu wa Utawala Kanda Maalumu Dar es Salaam pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Costantine Massawe anakwenda kuwa Mkuu wa Oparesheni wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Mabadiliko hayo ni ya kawaida kwa mujibu wa Sheria,  kanuni na taratibu za Jeshi la Polisi.

 Imetolewa na:
Advera Bulimba-SSP
 Msemaji wa Jeshi la Polisi (T)

 Makao Makuu ya Polisi.

Thursday, February 18, 2016

NECTA:TAZAMA MATOKEO KIDATO CHA NNE 2015

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
 
<<<<<Matokeo CSEE 2015>>>>>>

PIA TAZAMA MATOKEO YA
<<<<<<Matokeo ya QT 2015>>>

Sunday, February 14, 2016

Official VIDEO | Darassa Ft. Rich Mavoko - Kama Utanipenda

Saturday, February 13, 2016

magazeti ya leo jumapili february 14 2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
 

IDADI YA WASOMAJI